Pageviews all the time

INYANDIKO ZO MU BUBIKO. Rwanda-Tanzania.Iterana amagambo no kwishishanya hagati y'ibihugu byomi birakomeje!/NKUSI Yozefu

                              Iyi nyandiko yahise bwa mbere kuri Shikama kuri 2/2/2014
Kagame avuga ko azica Kikwete

Itangazamakuru ryo muri Tanzania rikomeje kugaruka ku byanditswe n'ikinyamakuru leta ya Tanzania yita ko ari icya Leta y'U Rwanda "the News of Rwanda". Uyu munsi ku cyumweru tariki ya 2 Gashyantare, ikinyamakuru Mtanzania cyo kirabona ko uku gushyamirana hagati ya Kagame na Kikwete, gushobora gukurura intambara hagati y'ibihugu byombi.

Mu cyumweru gishize, urubuga" The News of Rwanda" rwa leta ya Kagame, rwari rwatangaje ko Kikwete yabonanye na Rukokoma Twagiramungu, abarwanashyaka ba RNC nka Rudasingwa, intumwa za FDLR. ibi byose Tanzania ikaba ibihakana yivuye inyuma ndetse ikavuga ko kuri iyi minsi bavuga ko Kikwete yabonanye n'aba bantu, we yari mu nama i Davos mu Buswisi.

Nta gushidikanya ko mu ijambo ejo kuri 3/2/2014 Perezida Kikwete azageza ku baturage be ba Tanzania, azavugamo n'ibyo umubano we na Kagame. Tuzaba tuhabababereye.

Soma hasi aha inkuru irambuye ya Mwananchi.co.tz  mu rurimi rw'ikiswahili.

_______________________________________________________________________

Tanzania itapata nini kwa kuihujumu Rwanda?





Rais wa Rwanda Paul Kagame akisisitiza jambo.Picha na Maktaba 
Na Mhariri Wetu



Posted  Jumapili,Februari2  2014  saa 3:0 AM
KWA UFUPI
Pasipo kuthibitisha au kuonyesha vyanzo vya tuhuma hizo ambazo Serikali ya Tanzania imesema hazina msingi wowote, Gazeti hilo la ‘The News of Rwanda’ limeonyesha wazi kwamba, huenda limebeba ajenda ya siri inayosukumwa na baadhi ya wanasiasa nchini humo ya kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.Serikali mwishoni mwa wiki ililazimika kukanusha vikali habari iliyochapishwa na gazeti la Serikali ya Rwanda kwamba Rais Jakaya Kikwete anavisaidia vikundi vya waasi nchini humo kuihujumu Serikali ya Rais Paul Kagame.
Pasipo kuthibitisha au kuonyesha vyanzo vya tuhuma hizo ambazo Serikali ya Tanzania imesema hazina msingi wowote, Gazeti hilo la ‘The News of Rwanda’ limeonyesha wazi kwamba, huenda limebeba ajenda ya siri inayosukumwa na baadhi ya wanasiasa nchini humo ya kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Tamko la Serikali kupitia kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Francis Mwaipaja limesema Rais Kikwete amesikitishwa na habari hizo za uongo na kusema zinaweza kujenga chuki na kuwachanganya wananchi wa nchi hizo jirani na rafiki.
Jambo ambalo tunadhani Serikali ya Tanzania itahitaji ufafanuzi kutoka Kigali ni msimamo wa Serikali ya Rwanda kuhusu tuhuma hizo zilizochapishwa na gazeti hilo inalolimiliki. Itakuwa vigumu kwa Serikali kujenga hoja kwamba gazeti lake lilichapisha tuhuma hizo nzito pasipo serikali yenyewe kujua na pengine kuridhia.
Tunaposema hivyo hatuna maana kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa imara siku zote.
Mwaka uliopita uhusiano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili ulidorora baada ya Rais Kikwete kumshauri Rais Kagame kufanya mazungumzo na vikundi vya waasi vya FDLR na RNC ili kupata maridhiano, lakini Rais huyo aliuchukulia ushauri huo kama matusi kwa nchi yake na kusema hawezi kukaa pamoja na watu aliodai walifanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya 800,000 waliuawa.
Vilevile, kitendo cha majeshi ya ulinzi ya Tanzania mwaka jana kushiriki kupambana na kukisambaratisha kikundi kilichokuwa kikihusishwa na Serikali ya Rwanda cha M23, ambacho kilikuwa kikiendesha hujuma dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kilimkasirisha sana Rais Kagame.
Hali hiyo ilisababisha Kenya, Uganda na Rwanda kuitenga Tanzania katika baadhi ya mambo muhimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Hata hivyo, wakati juhudi za kurejesha uhusiano baina ya nchi hizo mbili zikionekana kuzaa matunda, ndipo gazeti hilo lilipoibuka na habari hizo za kutunga dhidi ya Rais Kikwete na serikali yake kwa lengo la kuweka mazingira magumu ili kukwaza juhudi hizo.
Kama tulivyosema hapo juu, wapo watu wanaofaidika inapokuwapo hali ya kutoelewana baina ya viongozi wa nchi hizo jirani na rafiki.
Tunasema hivyo, kwa sababu inawezekanaje gazeti limtuhumu Rais Kikwete kwamba katika nyakati tofauti mjini Dodoma na Ikulu jijini Dar es Salaam alikutana na Waziri Mkuu wa zamani wa Rwanda, Faustine Twagiramungu pamoja na viongozi wa RNC na makamanda wa FDLR, wakati dunia nzima inajua kwamba wakati huo alikuwa Davos, Uswisi akihudhuria Mkutano wa Dunia Kuhusu Uchumi (WEF), ambapo alikutana na viongozi mbalimbali duniani, wakiwamo Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza, Niuck Clegg na Mkuu wa USAID, Rajiv Shah.
Tunashangazwa pia na madai ya gazeti hilo eti Tanzania imeanzisha taasisi ya kuwasaidia waasi wa Rwanda na ilitoa pasi za kusafiria kwa viongozi wa makundi ya waasi yaliyotajwa hapo juu. Tunaishauri Serikali kuchunguza chanzo cha tuhuma hizi za kuchonga. Hivi Tanzania itapata nini kwa kuihujumu nchi kama Rwanda?
source: Mwananchi
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------




No comments:

Post a Comment

Muvandimwe, nshuti ya SHIKAMA, turagushimira cyane umuganda utanga wo kubaka URWANDA rushya ubinyujije mu bitekerezo byawe( Komanteri). Kugirango turwanye urukungu rw'Agatsiko ni ngombwa ko buri komanteri ibanza gusuzumwa. Yohereze, irahita ijya ku rubuga mu minota mike niba idatandukira( kuvuga ibitajyanye n'inyandiko), itukana, cyangwa yuzuyemo uburere buke.

Wipfusha komanteri yawe ubusa ukoresha "ANONYMOUS", himba izina urikomeze kuko hari ibihembo mu Kuboza 2016 ku bantu 3 bazaba babaye indashyikirwa mu gutanga ibitekerezo. Dukomeje kubashimira ubwitange n'umurava muhorana. IMANA Y'I RWANDA ihorane namwe iminsi yose.

Dg NKUSI Yozefu
www.shikamaye.blogspot.com
Uharanire ko Ukuri gusimbura ikinyoma.
Email: mahoriwacu@gmail.com; tel: +4745564355